Blogger Widgets

July 17, 2013

Mrembo ambae ni Miss Tanzania Akiwa Nchini China Aamua Kufunguka kwa Kuwadiss Boyfriend Zake aliowahi Kudate Nao

Mlimbwende  aliyewahi kung’ara katika Shindano la Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kuangukia kimapenzi kwa mtoto wa Balozi wa Nigeria nchini China aliyemtaja kwa jina moja la Allen anayetaka kufunga naye ndoa. 


Akichati na mwandishi wetu, kwa njia ya mtandao, Rehema alikiri kuwa na mwanaume huyo ambaye ni mtu mzima na kweli ni mtoto wa balozi huyo.
 


“Nimechoshwa na masharobaro hivyo nimeamua kutulia na mwanaume huyo kwa sababu nimempenda na yeye anaonekana kunipenda,” aliandika Rehema.

Rehema ambaye kwa muda mrefu amekuwa nchini humo, alisema kwamba amekuwa akipata wanaume wanaomtumia na kumuacha lakini safari hii amepata mtu sahihi.

“Tumepanga kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mipango ya ndoa, hivyo nitarajieni huko muda si mrefu,” aliandika Rehema na kuongeza kwamba atafanya bonge la sherehe

No comments:

Post a Comment