Blogger Widgets

July 8, 2013

Msikilize Msanii M2 THE P akizungumza Juu Ya Mpango wa Kumuenzi Mshkaji Wake Albert Mangwea

Baada ya kuondokewa na kipenzi chake cha karibu (Ngwea), M2thep amesema yuko mbioni kuchora tattoo kubwa yenye sura ya Ngwea mgongoni katika kumkumbuka kwake, na kwasababu alipokuwa nae South Africa mara ya mwisho alimtakia kuwa anataka kuchora tattoo.

"Tattoo ya chozi hii niliichora kwasababu ya kuondokewa na mama yangu mzazi, hii inaashiria nilipoondokewa na mama yangu, then niliweza kuchora tattoo hii ya chozi, yaah nikachora tattoo hii ya chozi, nikachora tattoo ya music mkononi, ambapo mi ni blood ambae napenda sana music, nikachora melody kwenye shingo,then nataka kuchora tattoo kubwa ngongoni yenye picha yake, nadhani itakuwa ndio kumbukumbu yangu kubwa, ambayo ntaichora mgongoni, kichwa kizima cha Albert nitakichora, yaani nategemea hicho kitu kukifanya, yaani ntakapo tulia nadhani, ntakapotulia ntaweza kufanya hicho kitu, kwasababu sasa hivi yenyewe ndio nimeanza ku recover, na natoka toka sasa hivi na vitu vingi vinanihusu studio nini, ila nikipata muda ndio ambacho cha muhimu, yaani hata yeye mwenyewe kwanza kipindi anakuja soth africa alisema mwenyewe anataka kuchora tatto, lakini kwa bahati mbaya mpaka anaondoka hajaweza kuchora hiyo tatto ambayo alikuwa anaitarajia yeye wenyewe kuichora, ambacho mi ndio nitakachokifanya kumuenzi, ntachora tattoo kubwa mgongoni ambayo itakuwa na picha yake" amesema M2thep