Blogger Widgets

July 7, 2013

Mtoto Mzuri Mwingine aliyepigwa na 50 Cent Week IliyopitaKufuatia tuhuma za 50 Cent kumpiga Mama wa Mtoto wake Shaniqua Topmkins ambazo zimevuma sana kwa wiki hii ambapo pia rapa huyu ametumia nguvu nyingi sana kuzikanusha, Sasa mapya yameibuka baada ya Girlfirend wa msanii huyu ambaye wengi walikuwa hawamfahamu, Bibie Daphne Joy ambaye ni model kutoka Philipines kuibuka na kudai kuwa yeye ndiye mwanamke ambaye 50 aliingia katika ugomvi naye mwisho wa mwezi uliopita.
Mwanadada huyu kwa mujibu wa ripoti pia ameweka wazi kuwa, ana mtoto mmoja na 50 Cent na kwa sasa lengo lake kubwa ambalo anazingatia ni kuwa salama yeye pamoja na mtoto wake.
50 Cent kwa sasa amewekeza nguvu nyingi pamoja na wanasheria wake kujisafisha na kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha tuhuma hizi ambazo kwa mujibu wake hazina ukweli wowote.