Blogger Widgets

July 9, 2013

Refa auwawa Bazil na kukatwa kichwa na mashabiki baada ya kumchoma kisu na kumuua mchezaji. tunaomba radhi kwa video hii kama itakukwaza

Refa Otavio Jordao da silver (20) kutoka brazil auwawa kikatili na kunyofolewa kichwa baada ya kumchoma kisu na kumuua mchezaji Josenir Dos Santos Abreu (30) uwanjani katika mechi ya kienyeji iliyofanyika June 30. Moranhao, Brazil.
 inasemekana refa huyo aliingia katika ubishani na mchezaji Josenir baada ya kupuliza kipenga. baada ya kushindwana katika ubishi huo, refa alichukua kisu cha mfukoni na kumchoma mara nyingi na kusababisha kifo cha mchezaji huyo ambae alifia njiani akikimbizwa hospitali.
Baada ya tukio hilo watu walio na hasira na wanao aminika kuwa ndugu na marafiki wa mchezaji huyo, walimshambulia refa huyo, wakaanza kumpiga, wakamfunga na kumpiga na mawe kabla ya kumkata kichwa na kukitundika kwenye mti na baadae kukisimika katikati ya uwanja.
Mpaka sasa polisi wanamshikilia Luiz Moraes de souza (27) kwa tuhuma za mauaji hayo, ambae amekubali kumtukana refa huyo lakini amekanusha kumuua