Blogger Widgets

July 25, 2013

Shuhudia Baadhi Zawadi za Birthday Ya Kajala Zilizotumwa na Wafungwa Kutoka Segerea

 
Keki iliyotumwa na wafungwa katika ‘bethidei’ ya Mwigizaji Kajala Masanja.
Na Imelda Mtema
KATIKA hali ya kushangaza, baadhi ya wafungwa walio nyuma ya nondo za Gereza la Segerea a.k.a Segedansi, Dar, wametuma keki ya ‘bethidei’ kwa Mwigizaji Kajala Masanja ikiwa ni miezi michache tangu alipoachiwa huru baada ya Wema Isaac Sepetu kumlipia faini ya Sh. milioni 13.

 
Kajala akishika sahani ya keki kwa ajili ya kumlisha Wema.
Tukio hilo lilijiri Jumatatu iliyopita Julai 22, mwaka huu ambapo mwanadashosti huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa bila kutaja umri aliofikisha.
Kabla ya pati hiyo na zoezi la kukata keki ikiwemo iliyotumwa na wafungwa hao, iliyopangwa kufanyika wakati wa kufuturu, Kajala aliianza siku hiyo kwa kwenda kutoa misaada kwa watoto yatima.

 
Baadhi ya keki alizoletewa Kajala.
Huku akiongozana na rafiki zake, Kajala alikata keki yake ya  kwanza katika Kituo cha Watoto Yatima cha  Mitindo House Talent (MHT), kilichopo Msasani, Dar, kinachomilikiwa na  mbunifu maarufu wa mavazi, Khadija Mwanamboka.
Baada ya kukata keki mbili ambazo alikwenda nazo kituoni hapo, Kajala pamoja na wapambe aliongozana nao walikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Beautiful Onyinye au Madam Wema, Kijitonyama jijini Dar ambapo shughuli nzima ilichukua nafasi wakati wa futari.
Katika futari hiyo ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Kajala, walialikwa watu mbalimbali huku kukiwa na vyakula vya kila aina wakiwemo mbuzi wawili wa kuchoma.
Baada ya futari watu walihamia kwenye ukataji wa keki zilizokuwa mezani zipatazo kumi na tano kutoka kwa marafiki wa Kajala huku Wema akiwa amenunua keki tano kwa ajili ya ‘shostito’, wake huyo.
Katika keki zote, iliyowafurahisha watu wengi ni ile iliyotumwa na wafungwa wa Gereza la Segerea iliyokuwa imeandikwa ‘Happy Birthday Mkuu wa Nyapara From Segerea Crew 2013’ ambayo kila mtu aliyeisoma alikuwa akicheka na kuanza kumtania mwanadada huyo kuwa ni Nyapara.
Kajala alisema kuwa Keki hiyo kutoka ilimkumbusha maisha ya gerezani lakini pia alifurahi kuona watu aliokuwa nao lupango humo  kumkumbuka hivyo alifarijika kupita maelezo.
Kajala alitupwa gerezani wakati kesi yake na mumewe Faraji Agustino ya kutakatisha fedha haramu ikiunguruma ambapo baada ya hukumu, mwanadada huyo alitakiwa kwenda jela miaka mitano lakini alilipiwa faini na kurejea uraiani huku mumewe akienda ndani.