Eneo alilonunua Diamond katika Mtaa wa Kaprikoni-Kijitonyama jijini Dar.
WAKATI
Wema Isaac Sepetu akiongeza idadi ya magari kwa kununua mkoko wa maana,
zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemziba mdomo baada
ya kununua eneo kubwa ambalo ndani yake kuna nyumba tatu, jirani na
anapoishi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Ijumaa Wikienda lina maelezo
kamili.
Tukio
hilo lilijiri hivi karibuni Mtaa wa Kaprikoni-Kijitonyama jijini Dar na
kusababisha watu kupigwa na butwaa na kudai kuwa kweli ‘dogo’ ana jeuri
ya fedha kwa kitendo hicho cha kununua karibia mtaa wote huo.
Diamond.
Akizungumza
nasi baada ya kukamilisha kila kitu kuhusiana na ununuzi wa eneo hilo
ambalo kwa mujibu wake anatarajia kujenga jengo lenye ghorofa nne na
nyumba za kawaida tatu, Diamond alisema kuwa anajitahidi kuongeza idadi
ya mijengo anayomiliki kwa kuwa ndicho kitu cha thamani kuliko magari.
NA GPL
Mkoko wa Wema.
“Najua
(nyumba) zitanisaidia endapo muziki wangu utakosa soko. Mimi na mama
yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) tuliishi kwa dhiki sana na sasa kwa
kipindi hiki ambacho Mungu ananisaidia na kuniwezesha kupata fedha kwa
wingi, siwezi kuishi maisha ya anasa ya kununua magari ya kifahari,”
alisema.
Wema.
Katika
hali iliyotafsiriwa kuwa ni kumtunishia msuli Wema, jamaa alitupia
maneno: “Mimi siyo kama hao wanaokimbilia kununua magari ya kifahari ili
mradi waonekane wako juu kifedha.
Eneo alilonunua Diamond anayemiliki nyumba zaidi ya tano Dar lipo mtaa wa nne kutoka anapoishi Wema
No comments:
Post a Comment