Blogger Widgets

July 24, 2013

Siri Yavuja Kwa Alichokifanya Agness Masogange Siku Moja Kabla Hajasafiri Kwenda Sauzi na Kukamatwa na Madawa ya Kulevya


MAMBO aliyoyafanya Mwanadada anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuingiza dawa za kulevya nchini Afrika Kusini Agnes Jerald (Masogange) na mwenzake Melisa Edward, kabla hajaondoka kuelekea nchini humo,  yameanza kufahamika. Msanii huyo ambaye ni Video Quin wa muziki wa bongo fleva kabla hajaondoka ndani ya jiji la Dar es Salaaam,aliandaa sherehe aliyowahusisha zaidi ndugu zake wa karibu pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya.


                      Agnes Gerald (Masogange)  akiwa katika pozi, kabla ya kusafiri nchini Afrika Kusini na kukamatwa.
Katika hafla hiyo msanii huyo alionekana kuwa ni mtu mwenye furaha sana,Masogange alisema amejisikia kula pamoja na watu hao ili kutimiza furaha ya moyo wake,ingawa hakuweka wazi alikuwa na furaha gani,Siku iliyofuata baada ya hafla hiyo Masogange aliazima gari la mdau wake mmoja ambaye ameomba hifadhi ya jina lake na kuwa nalo kwa saa kadhaa,safari yake zaidi siku hiyo ilikuwa ni Sea View Hotel na alikuwa akipigiwa simu kwa namba alizozijua aliwajibu kuwa alikuwa na mazungumzo nyeti na mtu hotelini hapo na kwa namba asizozijua hakupokea.
Masogange aliposti picha kwenye Instagram akiwa yeye na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ wakila ‘bata’. Aliandika maneno mbalimbali kama; ‘libeneke la bata litaendelea nikirudi.’ Hakusema anakwenda wapi na lini atarudi.
Siku iliyofuata baada ya kuandika kwenye Instogram,Msanii ( Masogange) alifunga safari kwenda uwanja wa ndege akiwa ameongozana na Melisa Edward ambaye anadaiwa kukamatwa naye siku hiyo.


Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa akisoma listi ya watu waliokamatwa na dawa za kulevya nje ya nchi
Mmoja wa watu wake wa karibu alisema kuwa “Sina uhakika na lini mzigo huo uliingia au safari hiyo aliipanga, lakini kumbukumbu zangu zinaniambia mzigo uliingia Bongo Juni 29, mwaka huu, ukitokea nchini …( ),” alisema mtu huyo huku akisita kutaja jina la nchi hiyo.
“Mabegi yaliyotumika siku hiyo si haya ya kawaida yanayouzwa na machinga, unajua wabeba unga wanatumia mabegi yanayojulikana kwa jina la Hand Curter, juu yana zipu moja kubwa, ndani kuna zipu mbili ambazo wewe kuziona ufanye kazi. Begi moja linauzwa shilingi laki nne (400,000). Kama uwanja una zana duni za kukagulia, hawawezi kuona unga ndani,” alisema shuhuda huyo.
Baada ya kufikishwa mahakamani Masogange na mwenzake dhamana yao iko wazi lakini mpaka sasa msanii huyo na mwenzake hawajapata watu wakuwadhamini. “Huku dhamana iko wazi, ila kila mtu anaonekana kukwepa kuwadhamini. Sijui watu wanadhani atatoroka? Lakini nijuavyo mimi hawezi kutoroka kwa sababu paspoti yake inashikiliwa na serikali,” alisema mnyetishaji wetu aliye nchini humo.

                                                                           Agnes Gerald (Masogange).
Habari kutoka chanzo chetu kimoja nchini Afrika Kusini, kinaeleza kuwa mtu anayepatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya kwa kuuza au kubeba huhukumiwa kifungo cha maisha au kifungo cha miaka 20,hivyo baada ya Serikali kuyadaka madawa hayo, yamepelekwa kwa mkemia mkuu kwa ajili ya uchunguzi zaidi na majibu yatatolewa Agosti, mwaka huu.
Baada ya kufikishwa mahakamani Masogange na mwenzake dhamana yao iko wazi lakini mpaka sasa msanii huyo na mwenzake hawajapata watu wakuwadhamini. “Huku dhamana iko wazi, ila kila mtu anaonekana kukwepa kuwadhamini. Sijui watu wanadhani atatoroka? Lakini nijuavyo mimi hawezi kutoroka kwa sababu paspoti yake inashikiliwa na serikali,” alisema mnyetishaji wetu aliye nchini humo.

From:Habari Mpya

No comments:

Post a Comment