Blogger Widgets

July 13, 2013

Tamko Rasmi la Jay Z Juu ya Kuchoshwa kwa Tabia ya Rihanna Ikiwa kama Yeye Ndio Bosi wake wa Rock Nation

Boss wa Roc Nation, Jay Z amenawa mikono kuhusu tabia mbaya anazofanya Rihanna anaesimamiwa kazi zake na lebel hiyo kwa kuchelewa kwenye shows mara kwa mara na kuahirisha show kadhaa, uvutaji na ulevi uliopitiliza tabia ambazo zimeonekana kuwakera fans wake katika kipindi cha hivi karibuni.

Jigga ambae sasa hivi ameteka headlines zote kwa ukubwa wa album yake ya 'Magna Carta Holy Grail' amefunguka katika interview aliyofanya na radio ya Marekani HOT97. 

"Hiyo sio sehemu yangu..siwezi kuingilia, natoa ushauri pale ninapoombwa..hivyo tu." Alifunguka Jay Z alipoulizwa kuhusu kumsaidia Rihanna kurudi kwenye mstari akiwa kama Boss wake. 

"Naweza kutoa taarifa kisha maisha yenyewe yatajiendesha, life has to happen." Aliongeza 

kumekuwa na taarifa kuwa Roc Nation walimpa Rihanna onyo kwa njia ya maandishi mwanzoni mwa mwezi July mwaka huu kutokana na tabia yake.

Rihanna anaonekana kuingia katika dimbwi la tabia mbaya katika kipindi ambacho hayuko tena na Chris Brown, huenda ni stress zinamchanganya au ndo hivyo tabia haina tiba.