Blogger Widgets

August 9, 2013

Aliyekuwa Mshiriki wa Big Brother Selly Aja Na Mpya Juu Tukio alilolifanya la Kusex na Mshiriki Nando wakiwa Ndani ya Jumba la Big Brother


selly
 Alipotoka kwenye jumba la Big Brother Africa, mwakilishi wa Ghana, Selly mwezi uliopita aliahidi kumchukulia hatua za kisheria Ammy Nando kwa kusambaza habari ya uongo kumhusu.
Wiki mbili baada ya Nando kuondolewa kwenye shindano hilo, Selly amebadilisha mawazo yake.
Kwenye mahojiano ya na gazeti linalouza zaidi nchini Ghana, Graphic Ghana,Selly amesema hana mpango wa kumshtaki tena Nando kwakuwa Mungu ameingilia kati na kumpigania.
“Hapana, sitachukua hatua zozote za kisheria dhidi ya Nando sababu Mungu amejibu sala zangu na ameniokoa. Ameipigania vita yangu, na leo Afrika nzima imekuja kufahamu Nando ni mtu wa aina gani na hiyo ni hukumu tosha kwangu.
Tangu nimereja, nimekuwa nikimuomba Mungu kuingilia kati na kurudisha heshima yangu lakini kwa njia yake mwenyewe Mungu, amenionesha mimi ni mwenye haki.

Hata kabla Nando hajatolewa, niliambiwa na waandaji wa Big Brother nisichukue hatua yoyote ya kisheria dhidi yake na nilijiuliza ni vipi nitasafisha jina langu na kurekebisha heshima yangu iliyoharibiwa lakini Mungu alikuwa na mipango yake kwangu. Huo ulikuwa ni mchezo wa Nando kuniondoa kama mshindani mwenye nguvu lakini Mungu anayejua zaidi hakuniweka kwenye aibu,”alisema Selly.
Selly amesema ingawa hajasikia chochote kutoka kwa Nando baada ya kuondolewa, hakuwa tayari kukubali ombi lake la msamaha kama angemuomba.
“Sitamsamehe kamwe Nando kwa si tu kunidhalilisha mimi na familia yangu, nchi yangu na mpenzi wangu aliyeumizwa na maneno na fedheha muda wote huo. Ameniletea madhara makubwa kwenye heshima yangu na kile alichokifanya hakistahimiliki,”alisema.

“Kinachoumiza zaidi ni kwamba, sikuwa na fursa ya kujitetea mwenyewe humo kwasababu sikusikia chochote kile hadi pale nilipotoka na niliumizwa zaidi kwasababu sikujua jinsi mpenzi wangu alivyojisikia, niliporudi nyumbani nashukuru amekuwa nguzo imara nyuma yangu.”
Kwa sasa, Selly, ambaye jina lake halisi ni Selorm Galley yupo chini ya usimamizi wa kampuni ya ARV Media na yupo tayari kuingia tena kwenye uigizaji wa filamu.