Blogger Widgets

August 16, 2013

Check Aibu Nyingine Kuhusu Madawa ya Kulevya kwa Tanzania:Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya Hii mashine waliyoipasua na Kukuta Madawa

HAPA CHUMA HICHO KIKIWEKWA KATIKA MASHINE MAALUMU YA KUKATIA KUWEZA KUJUA KILICHOMO NDANI
HAPA KIKIWA TAYARI KISHAKATWA NA KUGUNDULIKA KINA UNGA KWA NDANI YAKE


 

Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa

katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.