Blogger Widgets

August 23, 2013

Check Kilichijili Mchana wa Leo Ndani ya Tabora,Diamond Platnum akiwa Front Line na Mrisho Mpoto.NI FURSA KWA WOTE

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,
 Diamond, akiwaimbisha washiriki wa semina
 ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo 
kwenye ukumbi wa Student's Center uliopo katikati 
ya mji wa mkoa wa Tabora, kushoto kwake ni Bwa. 
Marco Vingila kutoka shirika la TPSF.
Mghani mahiri wa mashairi hapa 
nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa 
msisitizo, masuala ya fursa mbalimbali 
zinazopatikana katika suala zima la
 ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya 
Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa Student's Center,
 uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora. 
Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group, 
imefadhiriwa na shirika la NSSF; Zantel, 
MaxMalipo, Lake Oil. 
Baadhi ya Wasanii wa muziki wa 
kizazi kipya wakishiriki semina ya 
Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye 
ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa
 mkoa wa Tabora mapema leo, kutoka kulia ni 
Msanii Godzilla, Baba Levo, Amin, Stamina na wengineo.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa 
kampuni ya mafuta-Lake Oil, Bw Ben Temu
 akizungumza kwenye semina ya Fursa,
 ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali 
ikiwemo suala la vijana kuwa wenye moyo wa 
kujituma na kutokata tamaa, alieleza kwa kuwataka 
vijana wawe wavumilivu na kutoka tamaa
 kwa kila fursa wanayokumbana nayo,badala yake
 waitumie vizuri katika suala zima la kujikwamua 
na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo
 iliyoandaliwa na Clouds Media Group, imefadhiriwa na 
shirika la NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake Oil. 
Semina ya Fursa ikiendelea mapema leo 
ndani ya ukumbi wa Student's Center katikati 
ya mkoa wa Tabora mapema leo. Semina hiyo
 iliyoandaliwa na Clouds Media Group, 
imefadhiriwa na shirika la NSSF;
 Zantel, MaxMalipo, Lake Oil. 
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, 
Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya
 fursa alizozipata mara baada ya kujiunga na
shirika la NSSF, mbele ya Washiriki wa 
Semina ya Fursa (hawapo pichani), kulia kwake ni 
Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bw. Salim
 Khalfan akimsikiliza kwa makini. Semina hiyo
 iliyoandaliwa na Clouds Media Group, imefadhiri
wa na shirika la NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake Oil. 
Mwakilishi wa Shiriki la NSSF kutoka 
Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim 
Khalfan akielezea fursa mbalimbali zinazopatika 
mara mtu yeyote anayejiunga ama amejiunga na 
NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyeote 
atakayejiunga na shirika hilo atanufaika na 
mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,
mikopo na mengineyo lukuki yanayopatikana 
ndani ya shirika hilo.Semina hiyo
 iliyoandaliwa na Clouds Media Group
,imefadhiriwa na shirika la NSSF;
Zantel,MaxMalipo, Lake Oil. 
Baadhi ya Wakazi wa Tabora wakifuatilia
 kwa makini semina ya ujasiliamali iliyokuwa i
kiendelea ndani ya ukumbi wa Student's Center 
katikati ya mkoa wa Tabora mapema leo.
 
Picha ya pamoja, kiukumbusho zaidi, Msanii
 Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Diamond.
Mmoja wa akina Mama wajasiliamali 
kutoka mkoa wa Tabora,Flora Zakaria 
akiwa na bidhaa zake alizozitengeneza 
yeye mwenyewe kama mjasiliamali,akiuza ndani
 ya semina ya Fursa.semina hiyo ambayo 
imewahusisha wadau mbalimbali wakiwemo 
wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakazi 
mbalimbali wa mji wa Tabora, Wanafunzi 
kutoka vyuo mbalimbali.
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na 
Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge 
Mutahaba,Mkuu wa Wilaya ya Igunga 
( Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora),
Mh. Elibariki Kingu 
wakitazama paketi ya sabuti iliyotengenezwa
 na mjasiliamali aliyehudhuria semina ya Fursa,
iliyofanyika kwenye ukumbi Student's Center 
uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
Wadau wajasiliamali wakifuatilia kwa 
makini mada mbalimbali zilizokuwa
 zikijadiliwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji
 kutoka Clozds Media Group,Ruge Mutahaba,
akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya
 Fursa ndani ya ukumbi kwenye ukumbi Student
's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
Sehemu ya Meza kuu.Kutoka kushoto 
ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim 
 Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa
 (Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa 
Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani
 Singida,Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik
 Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group,
 pamoja na Ben Temu kutoka kampuni ya Lake Oil.
Baadhi ya Wasanii mbalimbali
 wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri
 kwenye semina ya Fursa,mapema leo mkoani Tabora.
Baadhi ya wakazi wa Tabora wakiwa
 kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi 
Student's Center mkoani Tabora mapema leo,
ambapo mada mbalimbali zimezungumzwa,
ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana,
mikopo,akiba sambamba na namna 
ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.

No comments:

Post a Comment