Blogger Widgets

August 16, 2013

Check Majina ya Watumishi walifukuzwa Kazi na Dr. Mwakyembe kwa Kumsaidia Agness Masogange Kusafirisha Madawa South


Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuwafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agness Gerald na mwenziye Mellisa Edward kupitisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine "TIK" au "Meth" au "USAN" kilogramu 180 kuelekea Afrika Kusini Julai 5, ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha O. R. Tambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya.

Waliofukuzwa ni   Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed ambao walihusika katika kuwasaidia Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa


No comments:

Post a Comment