Blogger Widgets

August 16, 2013

EXCLUSIVE : FEZA afunguka kuhusu Ukweli wa Mapenzi Yake napenzi na O'neal na bifu lake na Pokello

Mwanadada Feza Kessy aliyeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Big Brother Africa The Chase amefunguka kuhusu mambo mbalimbali yaliyotokea mjengoni ikiwa pamoja na hatima ya mapenzi yake na mshiriki kutoka Botswana O'neal.

Feza amesema mpaka sasa bado hawajazungumza kwa kina na mpenzi wake huyo kuhusu maisha baada ya Big brother japo anakiri kuwa kwa umbali uliopo ni nchangamoto kubwa kwao ambayo watakapopata muda watazungumza kwa kina.

Amesema wakati anaingia kwenye jumba la Big Brother alikuwa Single lady na ndio maana haikuwa tatizo kuangukia kwenye mapenzi na O'neal japo pia anakiri kuwa amevunja ahadi aliyoiweka wakati anaingia mjengoni ya kutokuwa na mpenzi ndani ya jumba.

Ameendelea kufunguka kuwa wakati wakianza mapenzi na O'neal kila mmoja alikuwa na wazo kuwa mwenzake anamtumia kwaajili ya kupata mkwanja unaotolewa kama zawadi unaofikia kiasi cha dola laki 3 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 450 za ki Tanzania,lakini kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda wakagundua kuwa wanapendana.

Feza akiendelea kufanya yake,..sijui ana chart na shemeji O'neal....


Mie,Feza na Cliford Mario Ndimbo

Akizungumzia bifu
lake na mshiriki kutoka nchini Zimbabwe Pokello,Feza amesema binafsi hana bifu na mwanadada huyo lakini mshiriki huyo wa Zimbabwe ndio ana bifu na yeye kiasi cha kutishia wakikutana anaweza kumfanya kitu mbaya,kitu ambacho haofii na atakuwa tayari kusalimiana naye bila kumpa nafasi ya ukaribu lakini hatakuwa adui yake.
Feza amefichua siri ya ugomvi wao kuwa ni mshiriki kutoka Ghana Elkem ambaye mwanzoni wakati wameingia kwenye jumba mkaka huyo alimweleza hisia zake za kumtaka kimapenzi lakini yeye akamchomolea na baadaye wakati mchezo ukiendelea alipomuhamisha Pokello(Swap) ikazidisha bifu ambalo mshiriki huyo wa Zimbabwe aliona ni kama ametenganishwa na mpenzi wake kwa makusudi.
Mshiriki huyo wa Tanzania hakuacha kuzungumzia jinsi alivyozimiss Chips Mayai(zege),na miezi mitatu ilivyomfanya azoee kuzungumza lugha ya kiingereza zaidi kuliko Kiswahili kwasababu ilikuwa ni lazima kuzungumza kiingereza na alionywa mara kadhaa kwa kuzungumza kiswahili na mshiriki kutoka Tanzania Nando ambaye anamuita mdogo wake.

From:MamuAfrica