Blogger Widgets

August 9, 2013

Hatimaye Jina La Mtoto wa Flora Mvungio na H Baba LapatikanaMwigizaji anayetarajia kujifungua hivi karibuni, Flora Mvungi amesema kuwa wamekubaliana na Mume wake H-baba kumpa jina la Tanzanite mtoto wao huyo anayetarajia kujingua hivi karibuni.
Flora alisema mumewe alichagua jina hilo kwa sababu mtoto wao huyo anatarajiwa kufahamika kimataifa kutokana na umaarufu atakaokuwa nao na ikizingatiwa kuwa madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania pekee.
Akinukuliwa na GPL flora alisema “Kama nikijifungua salama awe mtoto wa kiume au wa kike ataitwa jina hilo na atakuwa tofauti sana na msanii wa muziki anayejiita Tanzanite kwa kuwa yule hilo siyo jina lake halisi bali ni a.k.a tu,” alisema Flora.
Flora na H: Baba walifunga ndoa hivi karibuni na wakati wowote wanatarajiwa kupata tunda lao la kwanza kwani Flora ni mjamzito.