Blogger Widgets

August 27, 2013

Huyu Ndio Candice Mchumba wa Mshiriki wa Big Brother Kutoka Afrika Kusini Angelo,Ambaye wanatarajia Kufanya Tukio Kubwa Hivi Karibuni

Shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’ limemalizika jana usiku lakini drama zilizotokana na reality show hiyo ndio kama zimeanza rasmi nje ya jumba hilo. Jana masaa machache baada ya mtoto mzuri Dillish kutangazwa mshindi wa $300,000, kuna tetesi zilianza kusambaa katika mtandao wa kijamii wa twitter kuwa aliyekuwa mpenzi wa mshiriki wa Nigeria Beverly, Angelo amemchumbia mpenzi wake wa muda mrefu Candice Arends wa Afrika Kusini.
AngeloCandicePromiseRing2_that1960chickdotcom-copy
Tetesi hizo zilizoendelea kusambaa mpaka kwenye blogs uliambatana na picha ya wapenzi hao (Angelo na Candice) wakiwa wamekumbatiana kwa furaha huku Candice akionyesha kidole cha mkono wake wa kushoto kinachotumika kuvaa pete ya ndoa, kikiwa kimevishwa pete.
Angelo-href-naijavibe.net-1
Baada ya taarifa hizo kusambaa mtandaoni, blog moja ya Nigeria ‘that1960chick’ imeandika kuwa walifanya jitihada za kupata picha ya kidole cha Candice (closeup) na kuionesha vizuri pete aliyovishwa, lakini wao wanadai kuwa Angelo hajamchumbia Candice na kuongeza kuwa alimvisha pete ya ahadi ‘promise ring’ ambayo pia hufahamika kama (pre-engegement ring).
AngeloCandicePromiseRing_that1960chickdotcom-copy

Mtandao huo umeendelea kusema kuwa ukweli juu ya hali ya mahusiano ya Angelo na Candice ulianza kujionesha baada ya dada wa Candice kuanza kumshambulia Angelo kwenye twitter jana baada ya Angelo kumkumbatia na kumbusu Beverly katika live show ya fainali.
Whatever the truth is, huu utakuwa ni wakati mgumu sana kwa Beverly ambaye alijitoa na kuliwa tunda lake ‘live’ na Angelo huku Waafrika wakishuhudia kupitia TV zao, na bado pamoja na kufika fainali amezikosa $300,000 na sasa anakutana na habari na picha za mpenzi wake Angelo ambaye ni jana tu walipoonana wamekumbatiana na kukiss tena Live katika fainali hizo, kuwa amemvisha pete Candice, hiyo inaitwa double loss, wait! namaanisha DOUBLE LOSS! Pole ‘mwaya’ Beverly kama ni kweli.