Blogger Widgets

August 27, 2013

KAMA ULIKUWA HUJUI:Hii Ni Moja ya Fadhira Kubwa Aliyoifanya Wema Sepetu Kwa Marehemu Albert Mangwea


mirror

Asali


h-baba

dogo-janja

barnaba

wema2

wema

  Kama Ulikuwa Hujui Msanii Mirrow ni Mmoja wa Wasanii walikuwa wanaunda Kundi Moja na Marehemu Albert Mangwea Deja Vuu Music Ambapo Mipango ya Marehemu Ilikuwa ni Kuwatoa Wasanii Wachanga"Upcoming Artist" Akiwemo Mirror
Kwa Tukio Hili la Wema KumManage  Msanii Kama Mirror Hiyo ni Fadhira Kubwa Kwa Wema Sepetu Kwa Marehemu Albert Mangwea na Kumfanya Msanii Mirror Kuendeleza Ndoto zake.
Wasanii wanaokuja kwa kasi katika muziki wa Bongo flava hapa Tzee Mirrow pamoja na Asali jana waliweza kukonga nyoyo za mashabiki wao walipopanda Jukwaani.
Mirrow na Asali ni wasanii wanatoka katika kampuni ya Endless Fame ambayo ipo chini ya Mwanadada mahiri Wema Sepetu.
Katika uzinduzi huo wasanii wa Endeless Fame walitambulisha nyimbo zao mpya ambazo ziliwagusa mashabiki waliofika katika Club ya Bilicanas, pamoja na uzinduzi huo CEO wa Endless Fame Wema Sepetu alipanda Jukwaani kwa ajili ya kunena na mashabiki wake, ili waweze kuwapokea wasanii wanaotoka katika kampuni yake.
Uzinduzi wa nyimbo mpya za Mirrow na Asali ulisindikizwa na wasanii mbalimbali kama vile, Mwana FA, H.Baba, Country Boy, Barnaba, Mao, TID, Nyandu Tozi, Hassani Mapenzi.
Picha na Habari kwa hisani ya BaabkubwaMagazine.com