Blogger Widgets

August 20, 2013

Kifo Cha Loveness Love Diva wa Clouds FM


diva
 Ikiwa ni asubuhi nyingine ya Jumanne (August 20) baada ya kufika ofisini na kupitia huku na kule kuona nini kipya cha kukufaa, nikaingia Instagram na kukutana na ujumbe mrefu katika akaunti ya staa wa Ala za roho ya Clouds Fm, the one and only Diva Loveness Love.
Kidogo ilinibidi nichukue sekunde kadhaa kuipitia vizuri sababu kidogo imenishitua kama ambavyo imewashitua waliocomment pia, sababu kaandika vitu ambavyo huwa havizungumziwi sana kutokana na ukweli kuwa hakuna anayependa kitu chochote kinachohusiana na kifo.
Hiki ndicho alichokiandika Diva:
‘Kuna Siku Nitakufa na Wala sitoamka. Sitainuka…. Nitaanguka Nitakwenda. Ntawamiss Ndugu Zangu, Ntawamisi Mashabiki wangu. Ntam miss Babu yangu Tanga. Ntamiss vitu Vingi. Safari yangu itafika and The rest will be such a history. Kuna watu watakuwa wana haraka sana ya kuandika RIP DIVA. Kuna watakaofurahi na kuna wataolia sana. Sitaki Ku imagine how my lil sisters watakavyokuwa.
Sitaki Ku imagine any of that. Sitaki Ku imagine sehemu ntayozikiwa Ila Tanga Is My home. ntafurahi nikizikwa karibu na Kaburi ya Bibi yangu. i love her . i wanna Be close to her. life is top short that no one knows what we really fighting inside. Wakati Umelala mie Siku zote huwa nawaza. Nawaza Siku ya Kifo Changu’.
From:Bongo5