Hatimaye mwanadada Elizabeth Michael
(Lulu) yupo teyari kuachia filamu yake ya kwanza toka atoke jela, filamu
aliyoipa jina la Foolish age inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 30
mwezi huu.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii leo mchana lulu aliandika.
“Nina kila sababu ya kumshukuru
Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku
nitakayozindua movie ya mpya ya FOOLISH AGE....hatimaye narudi
kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI
CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY
DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki
wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....
Filamu hii inasambazwa ka kampuni ya PROINPROMOTERS.
Huu utakuwa ni uzinduzi mkubwa wa filamu
nchini baada ya msanii wa upande wa muziki wa kizazi kipya Diamond
Platnumz kufanya shoo kubwa ya mziki kwenye ukumbi mkubwa na maarufu wa
mlimani city jambo ambalo sio la kawaida kwa wasanii wa filamu na muziki
hapa nchini
No comments:
Post a Comment