Hit
maker wa Sio Mimi aka Pombe yangu, Madee amesema hadi sasa ameshaingiza
zaidi ya shilingi milioni 130 kutokana na show mbalimbali alizopata
hivi karibuni tangu aachie wimbo wa huo.
Madee
amesema pamoja na show za kawaida, makampuni ya simu yameshamsainisha
show zaidi ya 12 ambazo zimekuwa zikimpa mkwanja wa nguvu.
Akiongea
na Bongo5, Madee ambaye atatumbuiza kwenye show ya Serengeti Fiesta
2013 mjini Singida leo, amesema pia muziki wake umetoa fursa kwa vijana
wa Tip Top Connection ambao amekuwa akifanya nao kazi katika show
mbalimbali.
“Nimekua
nikiingiza Milioni 2 hadi 3 kwa wiki kutokana na Pombe Yangu. Ni
tofauti na awali wakati tunaanza muziki kwa sasa ukifanya wimbo ukawa
mkali basi ujue pesa zipo zinakusubiri. Pamoja na hayo wimbo ya Pombe
Yangu umetoa fursa kwa vijana ambao
nakuwanao kwenye show zang. Filamu ya “Pombe Yangu” pia imeajiri
vijana,watu wametengeneza T-Shirt ‘Nani kamwaga Pombe Yangu’. Hiyo ni
fursa wameitumia kupitia Pombe Yangu, alisema Madee.
No comments:
Post a Comment