Blogger Widgets

August 16, 2013

Picha Mbalimbali zikionesha Jinsi mwanamke aliyebakwa na Kuchomwa Kisu Sehemu za Siri.INATISHA


Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 amekutwa amekufa katika makaburi ya Majengo soko la mjini Kahama mkoani Shinyanga huku mwili wake ukiwa ametobolewa macho na kuonesha kupigwa na kitu kizito usoni.
Mwanamke huyo ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka alikuwa amevaa Blauzi nyeusi yenye madoa meupe, viatu vyenye urembo wa silva, mnene kiasi, mweusi na mwenye nywele ndefu.

Mwili wa Mwanamke huyo amegunguliwa leo majira ya saa sita Mchana baada ya watu waliokuwa wanachimba kaburi kuuona mwili huo pembeni ya eneo hilo na kutoa taarifa Polisi.
Kwa mujibu wa majirani wanaoishi eneo la makaburi hayo, tukio hilo linakisiwa kutokea usiku wa kuamkia jana huku baadhi ya kina mama wakisema kuwa walisikia sauti ya mwanamke akipiga mayowe katika eneo la mnadani.
 
Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo  Kaskazini Noel Mseven amesema amepata taarifa kutoka kwa wananchi na baada ya kufika katika eneo hilo walibaini kuwa sehemu za siri za mwanamke huyo ziliingiziwa kitu chenye ncha kali.
 
Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Mrakibu msaidizi wa Polisi Aziz Mayunga akitoa wito kwa wananchi kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.

MATUKIO KATIKA PICHA
 
MWENYEKITI WA MTAA NOEL MSEVEN AKIUFUNUA MWILI ILI WATU WAUONE.


 
MSEVEN AKIENDELEA KUWAONYESHA WATU MWILI HUO.
  
SAMAHANI KWA PICHA HIZI JAMANI,TUNAFANYA HIVI ILI WATU WAMTAMBUE MAANA HADI SASA HAJAPATA NDUGU.

 
HILI NDILO ENEO LA MAKABULI ALIPOKUTWA MAMA HUYO.


JESHI LA POLISI LIKIWA LIMEFIKA ENEO HILO KUUCHUKUA MWILI HUO.
 
WANANCHI WAKISAIDIANA NA POLISI KUUBEBA MWILI HUO.


 
MWILI UKIPELEKWA KUPAKIWA KWENYE GARI


 
MWILI UKIPAKAKIWA KWENYE GARI YA POLISI


 
KATIKA ENEO LA TUKIO MWILI UKIPAKIWA KATIKA GARI TAYARI KWA SAFARI YA MOCHWARI.


 
HILI NDILO KABULI LILIKOKUWA LIKICHIMBWA NA WATU WALIOUONA MWILI HUO.


 
MWILI UKIPELWA HOSPITALI

No comments:

Post a Comment