Blogger Widgets

August 7, 2013

PICHA:Paka Aingilia Kati shughuli ya Aunt Ezekiel Baada ya Kufuturisha

FUTARI KWA AUNT, PAKA AZUA SHESHE MASTAA WATOKA NDUKI

Hamida Hassan na Imelda Mtema
PAKA mwenye rangi nyeupe amezua sheshe nyumbani kwa msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita alipokuwa akiwafuturisha mastaa wenzake na watu wengine


Tukio hilo lilitokea wakati wasanii wakifuturu na kuwafanya watoke nduki na wengine kufikia hatua ya kumwaga futari zao kuto kana na hofu waliyokuwa nayo.


Waliokumbwa na mshtuko baada ya kumuona paka huyo ni Irene Uwoya, Vyonne-Cherly Ngatikwa na Devota Mbaga ambaye presha ilimshuka na kumfanya hereni zake zimvuke bila ya kujua.


Hata hivyo, paka huyo alitulizwa baada ya kutupiwa mifupa kitendo kilichorejesha utulivu katika eneo hilo.


Baada ya watu kumaliza kufuturu, dua ilisomwa huku watoto yatima wa kituo cha Magomeni, Dar wakionyesha ushirikiano ila Aunt alisikika akisema, kwa tukio hilo siyo bure.