Blogger Widgets

September 3, 2013

Check Picha za Show Aliyofanya Kanye west na Kulipwa Billion 4

'Kanye West akodishwa kutumbuiza katika Harusi' [One can hardly imagine this happenin] lakini hiki kitu kinawezekana kabisa long una mpunga wa kumtosha kufanya hivyo, and YES INDEED, kitu hiki kimemtokea rapa huyu mwishoni mwa mwezi ambapo alikwenda kufanya show katika Harusi huko Kazhakstan.

Kanye alitumbuiza wageni katika harusi katika ukumbi mmoja uliopo katika hoteli ya Royal Tulip, na hii ilikuwa ni katika harusi ya mjukuu Rais Nursultan Nazarbayev.Story kubwa kutoka tukio hili ni kiasi cha pesa ambayo Kanye amelipwa kufanya burudani hii, Dola milioni 3 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 4 za Kitanzania kwa kuimba kwa muda mchache tu.


Story kubwa zaidi katika hili pia ni maoni tofauti ambayo msanii huyu amekuwa akikumbana nayo kwa sasa hasa kutokana na kukubali kwenda kutumbuiza katika himaya ya kiongozi huyu ambaye ni Dikteta.