Blogger Widgets

September 6, 2013

Hii Ndio Sehemu Nzuri Kabisa Ambayo Litafanyika Lile Shindano la Miss World

Huu ndio ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano ambao Indonesia mabo utatumika katika Fainali za mwaka huu za Miss QWorld 2013. Ni ukumbi wa kisasa ambao una kila kitu ndani yake ikiwapo taa za uhakika, spika za sauti, na unauwezo wa kuchukua watu hadi 11,000 walio keti. 
Mwaka huu mhindano ya Dunia ya Miss World 2013 yanataraji kufanyika 28 Septemba katika ukumbi wa kimataifa wa stunning Sentul nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo wa Jakarta. Ukumbi huu umejengwa kwa namnaya kipekee na kuzungukwa na madhari ya kuvbutia ya safu za milima katika pande zote.  

Indonesia ni nchi ambayo huelezewa kama eneo zuri na kubwa duniani. Taifa ambalo linavisiwa zaidi ya 17,500, huku lugha zinazozungumzwa ni 300, wakazi milioni 240 . Indonesia ni nchi iliyo jaa utajiri wa utamaduni na historia, kauli mbiu yao ni  "Bhinneka Tunggal Ika" (Umoja katika Diversity).

No comments:

Post a Comment