Blogger Widgets

September 13, 2013

Hiki Ndio alichoongea Mama Yake na Albert Mangwea Kama Hela alizoahidi Mwana Fa kwenye Show ya Finest Amepewa au Laah!!

Mama mzazi wa marehemu Albert Mangwea, Denisia Costantine Mangwea, amelazimika kuzungumza na kuthibitisha kuwa ni kweli alipewa fedha na Mwana FA aliyeahidi kutoa asilimia 15 ya fedha iliyopatikana kwenye show ya The Finest, June mwaka huu.
IMG_0909 (533x800)
Hatua hiyo imekuja baada ya kuzuka tuhuma kuwa Mwana FA ambaye jina lake ni Hamis Mwin’juma hakutimiza ahadi hiyo.
Akiongea na gazeti la Mwananchi la leo MwanaFA alikiri kutoa ahadi hiyo.
“Nakiri kukosea jambo moja, nilipoahidi, niliongea na wanahabari lakini wakati wa kutoa, nilitoa bila kutangaza, na hii kutoa jamani ni moyo, haina haja kumtangaza mtu kwa kuwa umemsaidia au umempa pole,” Mwana FA ameliambia Mwananchi.
Aliongeza shilingi milioni 19.5 alizoingiza, alitoa shilingi milioni tatu na kuzikabidhi kwa mama yake Ngwair kwa kuziingiza kwenye akaunti yake ya benki ya Exim. Gazeti la Mwananchi limedai kuwa liliamua kwenda hadi Morogoro kwa mama huyo kuthibitisha kama kweli alipokea fedha hizo.

“Kabla hata ya arobaini, aliweka benki kisha akaja na mwenyewe, hakuna na waandishi kama wanavyofanya wenzake, alikuja mwenyewe tukaongea, na mara kwa mara tunawasiliana, wanataka kumtia doa kijana wa watu ni muungwana sana,” Mama huyo aliliambia Mwananchi.
Ili kuthibitisha mama huyo alitoa risiti aliyokabidhiwa na MwanaFA ikionesha kiasi cha fedha alichotoa na tarehe halisi ambayo fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti yake.
“Naomba kwa niaba ya familia niwathibitishie alitoa na mngemwacha kijana wa watu aendelee na shughuli zake, kwani alitoa kwa nia njema na ndiyo maana hakutaka kuitangaza sana,” aliongeza.