Blogger Widgets

September 11, 2013

Hili Ndio Gari la Kifahari Atakalopewa Msanii Baby Madaha na Kupewa Shillingi Million 50 za Kitanzania

Muimbaji na muigizaji wa filamu nchini, Baby Madaha amesainishwa mkataba na kampuni ya Candy n’ Candy Records ya Nairobi, Kenya ambayo pia ilimsanisha Mr Nice na Hussein Machozi.
1185920_713838211964007_392247732_n
Baby anadaiwa kuingia mkataba wa shilingi milioni 50 za Tanzania huku akipewa gari la kutembelea aina ya AUDI TT na kupangishiwa nyumba nzuri ya kuishi maeneo ya Kijitonyama, Dar es salaam.
2003-Audi-TT-3.2-DSG-lg
Gari aina ya Audi TT


Akizungumza na website ya bongomovies, Joe Kariuki ambaye ndiye mmiliki wa label hiyo alisema Baby Madaha anakubalika sana nchini Kenya na wanataka kumhamishia Nairobi, Kenya kwa muda wa mwaka mmoja ili wafanye kazi kwa ukaribu zaidi.
Baada ya kupata taarifa hizi Bongo5 ilimtafuta Baby Madaha ambaye alisema yupo njiani kuja Dar akitokea Kenya na akiwasili leo, yeye na wamiliki wa kampuni hiyo watafanya mkutano na vyombo vya habari.