Blogger Widgets

September 11, 2013

Huu Ndio Muonekano wa Snura wa Majanga na Vanessa Mdee(V-MONEY more Swaggs) na Wengine kwenye Show ya OZONTO

 Menina akifanya yake jukwaani.
 Vanessa jukwaani akiimba Closer
 Snura Majanga akitoa burudani
Walter Chillambo akiimba
  Mashabiki waliojitokeza wakishangilia 
 Fuse ODG akifundishwa kucheza kiduku na shabiki
Wasanii wa Marco Chali Foundation wakiwa katika picha ya pamoja.
*********************************************
MSANII wa muziki wa kileo kutoka nchini Ghana Fuse ODG, Azonto amewapagawisha mashabiki wake wa Bongo baada ya kuchanganya staili yake ya uchezaji Azonto pamoja na ile ya Kiduku ambayo ni maarufu ya hapa nchini, wakati wa shoo yake iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi, mwishoni mwa wiki.

Fuse ODG ambae anajulikana zaidi kama Azonto alipanda jukwanii majira ya saa tisa kasoro usiku baada ya wasanii wengine wengi kumaliza kutoa burudani. Ilikuwa ni baada ya kupanda kwa kundi la Tip Top Connection huku likiongozwa na msanii Madee pamoja na msanii Chid Benz ambae aliimba nao kama msanii rafiki.

Baada ya kumalizika kwa shoo hiyo kwa wasanii hao wa hapa nyumbani ndipo alipopanda msanii Azonto ambae alisikika akihamaisha kwa kutajan maneno ya kiswahili kama vile, Nawapenda, Mambo vip na piga kelele.

Msanii huyo kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwaweka karibu zaidi wapenzi wake wa burudani hasa pale alipowapandisha jukwaani vijana wawili kucheza nao Azonto na Kiduku.

Alianza kwa kuwachezesha Azonto na kisha muda huo huo aliwabadilishia muziki na kucheza nao kiduku huku mwenyewe akiahidi kuiendeleza zaidi staili hiyo.

Akizungumza baada ya onesho hilo alisema kuwa amefurahishwa na namna ambavyo wasanii na watu wa Dar es salaam walivyompokea na kuahidi kuwa ataiendeleza staili ya kiduku nakuitangaza zaidi.

"Mimi kwanza niliwahi kuja Tanzania na kufikia kule Arusha kwa mapumziko na kwa sasa nimekuja kwa kazi na nipo tayari kufanya kazi na wasanii wa Tanzania kwani mwisho wa siku sisi ni waafrika ambao tunatakiwa kusaidiana na kuendelezana" alisema Azonto.

Wasanii kama vile Madee, Tunda Man, Water Chilambo, Menina Atik, kundi la Navy Kenzo, B Heats, Mabeste, Eskide, Mapacha na wengineo wengi pia walitoa burudani safi siku hiyo