Blogger Widgets

September 13, 2013

Issue Mpya Mpya Iliyoibuka Baada ya Jana Kusadikiwa kwa Msanii Huyu Mrembo wa Bongo Movie Kukamatwa na Madawa ya Kulevya Nchini Brazil

MSANII wa maigizo ya filamu Aisha Bui aliyekuwa mke mwenzie na Amina Chifuta inasadikiwa kuwa kweli  amekamatwa nchini Brazil akituhumiwa kuwa na dawa za kulevya.

Taarifa za ndani zilizo na uhakika zinasema kuwa  Aisha Bui amekamatwa nchini Brazil wiki hii akihusishwa na biashara za dawa za kulevya na hatua za uchunguzi zinaendelea katika vyombo vya sheria ikiwemo mawasiliano ya karibu kati ya Serikali hizo mbili.

Mapema Dar es salaam leo Waziri wanchi ofisi ya waziri Mkuu sera na uratibu wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi alisema Serikali inafuatilia kwa karibu kesi zinazowahusisha Watanzania waliopo nje ya  nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za kulevya wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.

Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu ya watendaji  imetumwa nchini Afrika kusini hivi karibu ili kukutana na kina Masogange kujua undani wa kesi yao na imethibitika kuhusika kweli na tuhuma hizo ambapo inasadikiwa leo  kesi yao imesomwa rasmi na kusubiri hatua zaidi za kisheria.

Akizungumzia  taarifa za kukamatwa kwa mwanamichezo Kaniki na Matumla Lukuvi alisema taarifa  hizo zitatolewa ufafanuzi zaidi na Serikali baada ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka nchini  Ethiopia.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha kupambana na kudhibiti na dawa za kulevya Godfrey Nzoa alisema kati ya timu waliokwenda Afrika kusini ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye alifanikiwa kukaa kwa karibu na wafungwa hao akiwemo Masogange na kubaini kuna siri nzito mgongoni mwa Mwasogange hivyo inahitaji uchunguzi ili mkono wa sheria uweze kuwagusa wote wanaohusika na kutumia wasanii katika janga hilo.

“Ni kweli masogange na wenzie wamekamatwa na dawa aina za Ephedrine ambazo ndio zinazotengeneza dawa za kulevya na zinaruhusiwa kuingia nchi yeyote kwa kibali malaum kwani pia zinahusika kutengeneza dawa za kifua  na timu iliyotumwa na Serikali imeweza kuzungumza nao lakini haimaanisha kwenda kwetu gerezani tunawatetea au tutawasaidia hapana kwakua hawakutumwa kufanya baisahara hiyo haramu ila tunajaribu kuwa karibu ili kuona wanapata haki zao na kuweza kubaini waliopo nyuma yao na kweli tumefanikiwa mnyororo ni   mrefu tunaendelea na uchunguzi ili kujua wafadhili na mabosi zao tunawatiaje mikononi”alisema


Aliongeza kuwa ameshangazwa na kipato kidogo wanachopata wasanii hao akiwemo Masogange ambapo Afande Nzoa hakutaka kukiweka hadharani ili kupisha uchunguzi zaidi huku akiongeza kuwa  kufuatia sheri iliyopo wasanii hao kesi zao zitafanyika Afrika  kusini kwakua ndiko walikokamatiwa na endapo kuna mkataba wa ubadilishana wafungwa Serikali itaangalia njia ya kuwasaidia ili watumikie vifungo vyao nchini.

No comments:

Post a Comment