Blogger Widgets

September 3, 2013

Ndio Hiki Kinachozungumziwa na Watu Baada ya Diamond Kuachia Video Yake Mpya

Jana video ya muziki ya Msanii Diamond platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.

Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.

Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema sepetu kama “vijembe” kwakwe, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema “TUACHE TULALE” maneno ambayo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio liliotokea miezi kadhaa iliyopita.

Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata haihusiani nayo kwenye wimbo???


No comments:

Post a Comment