Blogger Widgets

October 16, 2013

Baada ya Norah Kuzungumziwa Sana Kwenye Media Kwamba Kapigwa Kibuti na Mpenzi wake!!! Sasa Aamua Kuweka Picha akiwa na Mpenzi wake Mpya


SIKU chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Nuru Nassor ‘Nora’ kumwagana na mpenzi wake Geofrey Kusila, sasa amezua gumzo baada ya kuibuka na mwanaume mwingine mtandaoni. Risasi Mchanganyiko limenasa picha ya Nora akiwa amepozi na mwanaume huyo ambaye jina lake halijapatikana huku pembeni kukiwa na mbwa, katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram ikisindikizwa na maneno: “...na mlivyosawigika kama huyu mbwa, mjipange nina hasira na nyinyi hadi Mungu anajua.”
Paparazi wetu alivyomtafuta kwa njia ya simu, Nora alisema: “Mimi ni mwanamke hivyo kuwa na mpenzi ni lazima na huyo uliyemuona ni mwanaume, hivyo haina haja ya kujibu na kuhusu anaitwa nani hiyo ni siri yangu, siwezi kuweka wazi jina lake kwa sasa.”