Blogger Widgets

October 27, 2013

Baba Yake Wema Sepetu Afariki Dunia.Check Hapa

Wema katika picha ya pamoja na mama yake pamoja na marehemu baba yake.
 Balozi Abraham Isaac Sepetu amefariki dunia mapema leo akiwa katika hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi alioupata hivi karibuni mjini Zanzibar. Balozi Sepetu, ambaye pia ni baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, hadi anapatwa na ugonjwa na hatimaye mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.
Habari kamili kushu msiba huu mzito ulio ikuta familia ya Sepetu zitawaijia hivi punde.

Wiki chache zilizo pita Wema alipost picha hizi za marehemu baba yake akiwa hospitali anaumwa na kumuomba Mwenyezi Mungu amsaidie aweze kupona.
Na leo hii muda mchache uliopita amepost picha hii na maneno "i LOVE YOU DADDY SEPETU WANGU... DAH.... 
Mabinti wengine wa marehemu  Sunnah na Tunnu nao wamepost ujumbe huu kupita ukurasa zao za Instagram na facebook.......