Blogger Widgets

October 18, 2013

Check Jinsi Diamond, Nay wa Mitego, Ommy Dimpoz, Lady JayDee na Mavoko Walivyotokelezea Kwenye Mchuano wa kipengele kimoja Kwenye Hizi Tuzo

 Mastaa wa muziki kutoka Tanzania Nay Wa Mitego, Ommy Dimpoz, Lady JayDee na Rich Mavoko wanachuana katika tuzo za Nzumari 2013 ambazo hutolewa nchini Kenya.

nzumari
Kipengele wanachochuana mastaa hao ni cha msanii bora Tanzania ‘Best Artist Tanzania’.
Nay wa Mitego na Ommy Dimpoz wameingia katika vipengele viwili, ‘Muziki gani’ ya Nay ikiwa imeingia katika kipengele cha pili cha wimbo bora Afrika Mashariki ‘Best Song East Africa’ ikichuana na ‘Tupogo’ ya Ommy Dimpoz na ‘Badilisha’ ya Jose Chameleone.
Best artist Tanzania:
1.Ney wa Mitego
2.Diamond
3.Ommy Dimpoz
4.Lady Jay Dee
5.Rich Mavoko

Best Song East Africa
1.Muziki gani – Diamond ft Ney wa Mitego
2.Mobimba – P unit
3.Badilisha – Chameleon
4.Tupogo- Ommy Dimpoz

Kupitia Instagram Nay amewashukuru mashabiki wake na media kwa kusapoti kazi zake mpaka kuingia katika tuzo hizo,
“Thnx kwa mashabiki na media zote zina nazo sapoti muziki wangu#966.Nimeingia ktk tunzo nchini kenya ktk category mbili wimbo bora wa mwaka east africa ambao ni muziki gani category ya pili msanii bora wa kiume tanzania.#966 tuombe Mungu izi zote mbili tuchukue.. Cku ya tuzo ni tar 23 mwezi 11..!!”


Tukio la ugawaji wa Tuzo hizo linategemewa kufanyika Novemba 11 huko Mombasa, Kenya.
Source: mashavuniversity.co.ke