Blogger Widgets

October 9, 2013

Check Mkataba Mpya Kati ya Said Fella na Shaa


Msanii wa kike kutoka Tanzania mwenye uwezo mkubwa wa kufanya muziki wowote 'Shaa' ametia wino kwenye mkataba wa miezi sita na Saidi Fella kupitia Mkubwa Na Wanawe. Saidi Fella amesema  kuwa mkataba huu ni wa muda mfupi na watafanya kazi tofauti na Shaa sababu anauwezo mkubwa wa kuimba na kufundisha muziki.

Saidi Fella amesema wamefanya mazungumzo na Aliyekuwa manager wa Shaa 'Master J' na wamekubaliana kuwa atafanya kazi na mkubwa na wanawe kwa misingi yao na baraka zote wamepewa.

Bab Tale amekuwa akifanya kazi na Shaa kwa muda sasa na kuhamia kwa Said Fella kuta msaidi zaidi Shaa kuteka soko la nyumbani zaidi. Shaa amekuwa moja ya wasanii Kutoka Tanzania mwenye mashabiki wengi nje ya nchi yake.

Awali Shaa aliwahi kufanya kasimamiwa na Ay Na Master J. I Hope hizi ngoma mbili kutoka kwa Shaa zitatisha sana hapa Tanzania, Moja amefanya na At na Nyingine Na Rapper Shetta.

Shaa amesema haya ni maamuzi mazuri na yataongeza sana mashabiki wa muziki wake Nyumbani.