Blogger Widgets

October 15, 2013

Exclusive: Kala Jeremiah apata shavu la kuwa balozi wa Pepsi Tanzania, aeleza vigezo vilivyotumika kumpa shavu hilo.Check Picha


Leo ni siku njema iliyoweka historia katika safari ya muziki ya rapper toka Rock City Mwanza Kala Jeremiah baada ya kupata shavu la kuwa balozi wa kinywaji cha Pepsi Tanzania.
Kala ameiambia tovuti ya Timesfm kuwa amesaini mkataba wa kuwa balozi wa Pepsi Tanzania na kwamba anafanya kazi zote ambazo balozi wa kampuni anatakiwa kufanya.
“Nimesainiwa rasmi kuwa balozi wa Pepsi Tanzania, kwa hiyo kuanzia sasa hivi nafanya kazi zote za kibalozi ambazo balozi anatakiwa kuzifanya katika kampuni.”Amefunguka Kala wa Mwanza.
Balozi huyo mpya wa Pepsi ametaja vigezo vilivyotumika kumpa yeye shavu hilo, “Kwanza wanaangalia tabia ya mtu,yaani kwamba hujawi kupigana na wala hujawahi kuwa na maskendo,lakini pia wanaangalia umati wa watu ulionao na watu wako wanakusikiliza kiaasi gani.”

Amewashukuru fans wake ambao ndio wamempa nafasi hiyo, kwa kuwa kigezo kimojawapo ni kuwa na umati unaokusikiliza, “Mimi nisema nawashukuru mashabiki wangu zaidi kwa sababu wao ndio wamenifanya leo niwe balozi wa Pepsi, kwa hiyo shukurani zangu za dhati ziende kwa mashabiki wangu ambao wamekuwepo kwa ajili yangu siku zote na wamenionesha mapenzi mpaka makampuni mengine wameona kwamba nina watu wengi ambao wananielewa, kwa hiyo ni hivyo.”
Biashara ya Muziki Tanzania inazidi kufanikiwa, makampuni yanawekeza kwa wasanii wa nyumbani. Sote tunaamini#NyumbaniNiNyumbani.
From:Times

No comments:

Post a Comment