Blogger Widgets

October 7, 2013

Gumzo alilozua Msanii Elizabeth Lulu Jijini Mwanza

                                               lulu 605
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameacha gumzo Jijini Mwanza alioweza kuongea na wakazi wa jiji hilo pale alipoelezea jinsi gani wazazi wanapaswa kuishi na watoto wao, Lulu ambaye kwa sasa yupo katika harakati ya kuhakikisha kuwa kizazi kilicho chini ya miaka kumi na nane kinakuwa tayari kukukabili changamoto za mihemko ya miili yao na yanayowakabili katika makuzi yao.Akiwa jijini Mwanza aliweza kutoa somo kwa wazazi kuwa makini na watoto wao kuhusu maisha ya kawaida na kuhakikisha wanawafuatilia katika masuala ya masomo na mienendo yao katika maisha ya kawaida ili kutambua kama kuna mabadiliko yoyote kutoka kwa watoto hao bila suala hilo kuwaachia walimu na wasaidizi wa kazi.

Mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Benjamin Masanja kutoka Mwanza ambaye pia aliweza kumshuhudia Lulu amesema kuwa ni binti mwenye akili na uwezo mkubwa wa kujieleza na kwa mwendo huu anaamini kuwa anaweza kuokoa kizazi kikubwa chenye mitihani mingi katika makuzi yake yanayokabiliana na changamoto za utandawazi.

“Lulu ni dira njema kwa wale wote ambao wapo katika umri mdogo na wanakabiliana vishawishi vingi kutoka kwa wavulana na watu wazima kabisa, lakini pia kwa vijana wa kiume nao kujikuta wakiingia katika madawa ya kulevya hata ngono,”anasema Masanja.

Lulu ambaye ni balaozi wa tamasha la filamu linalojulikana kwa jina la Dar Filamu Festival , kwa sasa anatumia muda wake mwingi kuwashauri vijana ambao wapo katika mabadiliko ya utoto kuelekea ukubwani ili wasiweze kujiingiza katika matukio yanayoweza kuwasababishia matatizo.