Blogger Widgets

October 8, 2013

Hali Iliyopo Muda Huu Ubungo Baada ya Mabsi ya Kwenda Mikoani Kugoma Kusafirisha Abiria

Mabasi yaendayo mikoani leo asubuhi yamegoma kufanya safari zake kama ilivyo ratiba zake za kawaida, kwa madai kwamba walikuwa kwenye mgomo. Mwandishi wetu John Chacha alipofika katika Kituo kikuu cha mabasi Ubungo alikuta mabasi yote yakiwa yamepakia abiria lakini hayakuwa yametoka kufuatia wamiliki wa mabasi hayo kuwakataza madereva kuyatoa mabasi hayo kama ilivyo kawaida. 

Mabasi hayo yamegoma kufuatia mgomo wa malori uliosababishwa na ongezeko la tozo la asilimia 5 katika mizani. 

No comments:

Post a Comment