Blogger Widgets

October 15, 2013

Haya Hapa Mazungumzo aliyoyafanya Jana Msanii Lulu na Salama Jabir Kwenye EATV

MSANII wa filamu nchini Tanzania Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la (Lulu) ameonyesha kufurahishwa na tukio la wanaume wengi wenye pesa nyingi kumtongoza na kumtaka kimapenzi kila kukicha, Akizungumka katika kipindi cha mkasi kinacho ongozwa na mtangazi wa Luninga ya EATV Salama Jabir na kurushwa kila Juma Tatu saa 3:30 usiku, Lulu amesema kwamba amatongozwa kila siku.
                                    Lulu akifurahia moja ya majibu yake kuwa anatongozwa sana

Lulu alisema kwamba pamoja na kwamba wanaume wengi wa kila aina na wenye pesa nyingi, wanamtongoza kila siku lakini pia anafurahia kupendwa na kwamba anapogundua kwamba anapendwa huwa anajisikia raha na mwenye rufaha zaidi.
"Nikweli ninatogozwa sana kila siku wanaume wananitongoza, lakini mimi binafsi ninapenda sana ku .....pendwa ninapogundua kuwa mtu flani ananipenda huwa najisikia faraja sana, inagwa ni vigumu saa kutambua kwamba kila anaye kutongoza atakuwa na mapenzi ya dhadi kwako"alisema Lulu huku akiwa mwenye furaha zaidi.
                                        Salama akimpa Lulu dole baada ya kuweka bayana kwamba anatongozwa sana.Picha zote na Habarimpya.com
Akifafanua zaidi kuhusu hali hiyo Lulu alisema, "hali hii iliongezeka sana nilipokuwa China (gerezani) na niliporejea Tanzania (uraiani) kasi ya kutongozwa ikazidi lakini mimi binafsi ninapenda sana kupendwa, na nikigundua kwamba ninapendwa huwa sifichi furaha yangu".
Katika mazungumzo hayo yalitawaliwa na maneno kama vile, China,ikimaanisha gerezani, kurejea Tanzania ikiwa na maana ya uraiani, huku akijaribu kukwepa kuzungumzia suala la kesi yake kwa madai kwamba atakuwa akiingia huru wa Mahakama.  

MSANII maarufu wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la (Lulu) amevunja ukimwa na kusema kwamba wakati alipokuwa akiishi kimapenzi na aliyekuwa msanii mwenzake wa filamu, Marehemu Steven Kanumba alikuwa akikerwa na mambo mengi.
                                   
Msanii wa filamu Tanzania, Lulu akizungumza mbele ya Kamera za EATV.
Akizungumka katika kipindi cha mkasi kinacho ongozwa na mtangazi wa Luninga ya EATV Salama Jabir na kurushwa kila Juma Tatu saa 3:30 usiku, Lulu amesema kwamba kipindi akiishi na Kanumba kimapenzi kuna mambo mengi alikuwa akifanyiwa na Marehemu Kanumba asiyoyapenda, ingawa yalikuwa na lengo la kumfundisha.
                                 Lulu akijibu akitoa ufafanuzi kuhusu suala la Kanumba kwa majonzi.Picha zote na Habarimpya.com
"Nilikuwa namchukia Kanumba, kwa sababu alikuwa akinibana nilikuwa na kosa uhuru, ingawa alikuwa na lengo la kunifundisha lakini mimi sikuyapenda na nikajikuta na mchukia kupita kiasi, lakini hivi sasa ndiyo naamini kwamba alikuwa akifundisha kwa sababu baadhi ya mambo aliyokuwa akinikataza, leo hii ndiyo naona uzuri na ubaya wake"amesema Lulu.
From:HabariMpya