Blogger Widgets

October 16, 2013

Ile Nyumba Mpya ya Rich Mavoko inayozungumziwa Ikiwa Bado Inajengwa Ndio Hii Hapa Na Gari Lake Likiwa Limepaki Pembeni

Muziki wa bongoflava sasa hivi umekua kazi rasmi na vijana wengi wanabadilisha maisha yao na kuyaweka kwenye level kubwa zaidi ya kiuchumi kutokana tu na show, mauzo ya nyimbo kwenye simu za mkononi pamoja na biashara nyingine.
Rich Mavoko yule staa wa ‘will you marry me’ ameongea na  kusema “Nyumba ipo Morogoro kwetu lakini baada ya kuweka wazi hizi picha mama yangu aliniambia nisifanye tena hivyo, kikubwa zaidi kanambia nisiwe na maisha ya matangazo kwanza nyumba yenyewe bado inamaliziwa so kwasasa hivi sipo tayari kuelezea sana kuhusu nyumba lakini ikiwa tayari wasomaji  watakua wa kwanza kuona kila kitu”
Nyumba ya Rich Mavoko inamaliziwa kujengwa huko Morogoro na maneno yake mengine ni kwamba ‘Natakiwa niseme asante kwa watanzania wote.. maana bila nyinyi nisingepata haya mafanikio”.
mavoko3
mavoko2
mavoko1