Blogger Widgets

October 20, 2013

Lulu awaombea Babu Seya na Papii Kocha washinde kwenye Kesi Inayosikilizwa Tena Tarehe 30 Kwa Kuwaandalia Hiki


Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘aka’ Lulu ambaye kwa sasa ameokoka amesema ana imani kuwa Mungu anaweza kufanya miujiza na Nguza Viking pamoja na mwanae Papii Kocha wakashinda rufaa yao inayotarajiwa kusikilizwa tena October 30 mwaka huu.
bb89f24a317111e3999722000a1fcf03_8
Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania waliotoa hukumu ya wanamuziki hao, linatarajia kupitia upya hukumu hiyo mwezi huu.
“Ninaamini Mungu yupo…anasikia,anaona na ndiye mwenye kuhukumu kwa Haki…!!!!Dua zangu ziko pamoja na Mzee Nguza na Papii Kocha…!hakuna linaloshindikana mbele ya Mwenyezi Mungu…Kama anaweza kutoa Jaribu basi yeye pia ndo mwenye Uwezo wa kufanya Njia ya kutoka ktk jaribu Hilo…!Mwenyezi Mungu awasimamie katika rufaa yenu,” aliandika Lulu kwenye Instagram na kuambatisha picha hiyo chini.
bd7f8de2383a11e3929322000a9e0719_8

Muigizaji huyo anayafahamu vyema maisha ya jela baada ya kukaa mahabusu kwa takribani mwaka mmoja kutokana na kesi ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba April mwaka jana.
Nguza Viking na wanaye watatu walihukumiwa na Hakimu Mkazi Addy Lyamuya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kifungo
cha maisha jela mwaka 2004.
Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa mwezi Februari, mwaka 2010 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam lakini Jaji Thomas Mihayo naye aliwatia hatiani na kuafiki hukumu ya Mahakama ya Kisutu.
Walikata tena rufaa katika Mahakama ya Rufani na safari hii, Jopo la majaji watatu — Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati — liliwaachia huru Nguza Mbangu na Francis Nguza baada ya kubainika hawakuwa na hatia, na kuamuru Nguza Viking na Johnson Nguza watumikie kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya Msingi kama ilivyohukumiwa na mahakama zilizotangulia.