Blogger Widgets

October 8, 2013

Maneno ya Msanii Rado Baada ya Kupata Ajari

              MSANII wa filamu na muziki Bongo, Simon Mwapagata ‘Rado’ amefunguka kuwa wasanii wenzake wanaounda Kundi la Bongo Movie walikuwa wanasubiri aage dunia ili watengeneze kamati za fedha na kunywa pombe.
Simon Mwapagata ‘Rado’.
Akichonga na paparazi wetu, Rado alisema alikuwa ni kiongozi kwenye kundi hilo lakini kwa sasa amejitoa kwani wasanii waliopo ndani ya kundi hilo ni wabaguzi na hivi karibuni alipata ajali ya gari lakini hakuna hata mmoja aliyemjulia hali.
“Nasikitika sana na siwezi kuwauliza kwa nini hawakuja kuniona walikuwa wanasubiri nife waje watoe michango na kuunda kamati za pombe, baada ya kuona kumbe kundi hilo ambalo na mimi ni mmoja wa waanzilishi linafanya hivyo nimeamua kujiengua.
“Kundi limegeuka kuwa genge la pombe, umalaya na kupiga vijembe. Nimeamua kujiengua na kukaa pembeni, mimi ni jeshi la mtu mmoja sasa,” alisema Rado.