Blogger Widgets

October 11, 2013

Mcheck Msanii wa Bongo Movie aliyevuliwa Nguo na Kushikwa Sehemu zake za Siri

Devota Mbaga kushoto
MSANII wa Bongo Movie, Devota Mbaga hivi karibuni alipatwa na kisanga cha mwaka baada ya kuvuliwa nguo na maofisa wa uhamiaji alipoenda Hong Kong, nchini China kwa ajili ya shughuli zake za kibiashara.Kwa mujibu wa staa huyo, alifanyiwa kitendo hicho cha kuvuliwa nguo zote na maofisa wa uhamiaji mara alipotua Uwanja wa Ndege wa Hong Kong na kumsachi kwa kuhofiwa kuwa amebeba ‘unga’.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Devota alisema baada ya kuvuliwa, alishikwa sehemu zake za siri kitendo alichokiita ni cha kidhalilishaji.
“Ilikuwa ni baada ya kugongewa pasipoti yangu nikaingizwa kwenye kitengo cha polisi wa madawa ya kulevya ambao walinitaka nivue nguo zote ili nikaguliwe,” alisema kwa masikitiko.
Msanii huyo alisema mbaya zaidi siku hiyo alikuwa katika mzunguko wake wa mwezi lakini maofisa hao hawakujali.
Kama vile haitoshi, Devota alisema kuwa, baada ya kumalizika kwa zoezi hilo maofisa hao walimchezea sehemu za kifuani huku wakimwambia kama hakutaka kufanyiwa hivyo angerudishwa alikotoka.
 “Kwa kweli nimeumia sana kwa kitendo nilichofanyiwa, nimeshinda nikilia kutwa nzima na kila nikikumbuka naumia,” alisema Devota.