Blogger Widgets

October 9, 2013

Mjini Haina Mwenyewe:Check alichofanyiwa Mtangazaji Benny Kinyaiya

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Mama Land, kinachorushwa na Runinga ya Clouds ya jijini Dar, Benny Kinyaiya hivi karibuni alikombwa vitu kadhaa kwenye gari lake na vibaka mara baada ya kupaki gari nje ya nyumba yake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kinyaiya alisema kuwa siku ya tukio saa nne usiku aliporejea nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni Dar, aliegesha gari nje ya geti na kuingia ndani kuchukua kitu kisha aendelee na mishemishe zake.  
Habari zinapasha kwamba, baada ya kuingia wezi hao walitumia fursa hiyo kuvunja vioo na kuiba redio na vitu vingine.
“Inauma sana kwani kilikuwa ni kitendo kama cha dakika chache tu, yaani kuingia ndani na kutoka tu tayari nimeshaibiwa, natamani hata nimkamate mmoja ili nimuoneshe mfano,” alisema Kinyaiya

No comments:

Post a Comment