Blogger Widgets

October 5, 2013

Moja ya Kitchen Party iliyovunja Maadili Baada ya Kuingiza Mashoga na Kuonesha Kila Kitu Hadharani


KATIKA miaka hii kumekuwa na utaratibu
 usiofaa katika sherehe za
Kitchen
 Party wa kuwahusisha mashoga.
Kutokana na utaratibu huo usiofaa kumefanya
 sherehe hizo kupoteza uhalisia.
Kwa tafsiri nyepesi, Kitchen Party ni
 sherehe ambayo hufanyika kwa lengo maalumu
 la kumpa vyombo vya jikoni binti 
anayekaribia kuingia kwenye ndoa kwa
 maana ya kuolewa.
Sherehe hii huambatana na mwaliko wa ndugu,
 jamaa na marafiki. Lakini pia huwa maalumu
 kwa ajili ya wanawake.
Lakini cha kushangaza hizi sherehe
 zimekuwa ni uwanja wa kualika wanaume
 wanaojifanya wanawake 'mashoga' ambao 
hufanya mambo ya aibu.
Mengine ni aibu kiasi cha kutotamkika,
 lakini ninaposikia au kuona hayo kwenye
 sherehe hizi huwa ninajisikia kichefu
 chefu.
Mashoga hawa hutumika kuonyesha mambo
 ambayo kimaadili hayapaswi kuonekana 
hadharani.
Mfano wa mambo ambayo kwa ufahamu wangu
 ninaona hayafai kuonekana hadharani, ni
 pamoja na kukata viuno hadharani, kuvua
 nguo na wakati mwingine hata kuonyesha
 namna tendo la ndoa linavyofanyika.
Wakati sisi tunakua ilikuwa ni mwiko
 kuona
 mwanamke au mwanaume akikata viuno
 hadharani kutokana na unyeti wa tendo 
lenyewe. Lakini leo hii mambo haya 
yamekuwa hadharani.
Hata nguo ya ndani ilikuwa haiachwi ovyo
 ovyo, kiasi kwamba hata unapokwenda
 dukani unamnong'oneza muuzaji ambaye
 naye huitoa kwa kificho isionekane. 
Lakini leo hii utamkuta mama mtu mzima
 mwenye maumbile makubwa  nyuma akiwa 
amemtanguliza shoga mbele huku anakata viuno
  huku, kaning'iniza nguo za ndani nje nje
 bila wasiwasi.
Ninaugua juu ya hilo kwa sababu ni
 vitendo vya aibu ambavyo havifuati
 maadili ukizingatia washiriki wanaweza
 kuwa mama, dada au shangazi zetu hivyo
 suala la rika huwa halizingatiwi.
Mbali ya hayo, ninachelea kusema kuwa
  mambo ambayo huonyeshwa na mashoga
 hao, huwa ni aibu.
Ukiangalia jinsi anavyofanya shoga na
 yeye ni mwanaume, ni aibu kwetu sisi
 wanawake kwa sababu wanaonekana ni wajuzi
 zaidi, hivyo wanawake huwa tunajitukanisha
 pasipo kujijua.
Jingine la kushangaza zaidi ni pale
 tunapokuwa mstari wa mbele katika
 kushabikia mambo ambayo hayana maana,
 tena kwa shangwe na vigelegele tukionyesha kufurahia mambo hayo.
Kwa upeo wangu, wakati binti anakaribia
 kuolewa kuna mafunzo ya ndani kabisa
 ambayo hupewa na bibi, shangazi au  somo
 ambaye ni maalumu kwa ajili ya kumfundisha
 namna ya kumtunza mume, usafi na kutunza
 familia pindi atapoingia kwenye ndoa yake.
Na baadaye sherehe za Kitchen Party 
hufuatia
 maalumu kwa ajili ya kumzawadia vyombo 
vya jikoni sambamba na  kuhitimisha kwa
 sherehe za kuagwa rasmi na familia, ndugu
 jamaa na marafiki.
Huo ndiyo utaratibu ninaoufahamu mimi.
 Lakini leo hii utaratibu huu umebadi
lishwa kiasi cha Kitchen Party kuwa
 mahali ambako hufanyika vitendo vinavyo
chochea vitendo vya kisagaji, ushoga,
 ulevi, matusi ya nguoni na wakati 
mwingine hata ugomvi.
Binafsi sipendezwi na hili kwakuwa lengo
 ni kujenga na si kubomoa. Je, kizazi
 kilichopo na kijacho kinajifunza nini?
Na inakuwaje kinamama watu wazima ndio 
wanakuwa mashabiki wa mambo yasiyo ya 
msingi? Je, mmerogwa au mnajitoa ufahamu?
 Ni lazima kuita mashoga?
Ifike mahali tuwe na hofu ya Mungu kwa
 kuzingatia maadili  kwa maana ya kwamba
 wanawake tunaweza, na hatuna haja ya
 kuita mashoga wanogeshe Kitchen Party
 ilihali si mahali sahihi kwao.
chanzo:daima.