Blogger Widgets

October 15, 2013

Noorah adai muziki hauna maana tena kwakuwa hauna manufaa katika maisha yake.Check Picha na Alivyozungumza

Rapper wa Chamber Squad, Noorah aka Babastlyez amesema hana hamu kubwa tena ya kufanya muziki kwakuwa haumnufaishi kwa chochote.
966142f9b3L
Akizungumza na DJ HAAZU katika kipindi cha Dundo cha MJ RADIO Arusha, Noorah ambaye hivi karibuni alifunga pingu za maisha, alisema muziki hauna faida kwake na kwa sasa anaufanya kama starehe tu.
“Maisha ni malengo, kitu hata kama unaweza vipi, hata kama watu wanakupenda vipi kwenye hicho kitu, kama hakina manufaa mazuri kwako, hakina maana kwako,” alisema Noorah.
“Mimi muziki kama naufanya, naufanya kwa starehe zangu tu, haya mambo ya kutoa single, ifanye hivi, biashara hiyo sasa hivi haipo kwangu.”

Noorah aliongeza kuwa muziki wa Tanzania una siasa nyingi kiasi ambacho hata wale wanaonekana wamefanikiwa hawana lolote.