Blogger Widgets

October 18, 2013

Picha Ikionesha Jinsi Wastara Alivyoumia Tena Mguu Huko Kenya

MWANADADA anayeendesha maisha yake kwa kuuza nyago kwenye filamu Bongo,  Wastara Juma ameumia mguu baada ya kuwekewa mwingine mpya wa bandia huko Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza na paparazi wetu siku chache baada ya kurudi Bongo, Wastara alisema aliumia wakati akifanya mazoezi ya mguu mpya aliowekewa ambapo kwa sasa anaendelea kuuguza jeraha hilo na amerudi mara moja kwa ajili ya Sikukuu ya Idd, ikimalizika atarejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Nimeshindwa kula sikukuu mbali na watoto wangu ndiyo maana nikaja mara moja japokuwa siko vizuri kwa sababu niliumia kwenye mazoezi ya kutumia mguu mpya huko Nairobi  na sasa nauguza kidonda lakini baada ya hapo nitarudi tena Nairobi kwa ajili ya matibabu,” alisema Wastara.
From:GPL

No comments:

Post a Comment