Blogger Widgets

October 28, 2013

Picha Zikionesha Jinsi Mh.Rais Jakaya Kikwete na Mkewe walivyoenda Kutoa Pole kwenye Msiba wa Balozi Isaac Sepetu

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Mama Salma Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu, wakati yeye na mkewe Mama Salma Kikwete (picha ya chini) walipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza Mori jijini Dar es salaam  kutoa pole. Balozi Sepetu alifariki dunia jana asubuhi kutokana na kiharusi na kisukari. Kwa mujibu wa duru za kifamilia marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano Oktoba 30, 2013 huko Mbuzini, Zanzibar.
Mama Salma Kikwete akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu, wakati yeye na mmewe Rais Kikwete (picha ya juu) walipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza Mori jijini Dar es salaam  kutoa pole.


Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu  enzi za uhai wake

Mwili wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu utafikishwa nyumbani kwake eneo la Sinza Mori lililoko jijini Dar es Salaam siku ya kesho Jumanne October 29, 2013 kuanzia saa sita za mchana na mwili huo utaanza kuagwa kwenye mida ya saa nane za mchana na baada ya kuagwa mwili huo utafanyiwa maandalizi ya kusafirishwa kwenda Zanzibar siku ya Jumatano asubuhi tarehe 30, October 2013 na mwili wa marehemu ukifika Zanzibar, Unguja utapelekwa  kanisani kwa ajili ya maombi pia utapumzishwa kwenye makazi yake ya daima eneo la Mbozini, Unguja siku ya Jumatano October  30, 2013
Balozi David Kapya akisaini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Balozi  Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake eneo la Sinza Mori jijini Dar es salaam leo Jumatatu October 28, 2013
Mke wa marehemu akiwa kwenye majonzi
Wema Sepetu akiwasiliana na ndugu na jamaa kwenye msiba wa baba yake marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo October 28, 2013

Picha na Ikulu