Blogger Widgets

October 28, 2013

Rado Azungumzia Kile Kilichoonekana Kwenye Tv Baada ya Kutaka Kumpiga Wema Sepetu "siku ile ningemtoa meno,”


STAA wa sinema za Kibongo, Simon Mwakipagata ‘Rado’ amefunguka kuwa Wema Sepetu ‘Madam’ aliponea chupuchupu kwani ilibaki kidogo amng’oe meno.


 
Wema Sepetu ‘Madam’.
Akizungumza na Stori, hivi karibu baada ya kukumbushiwa tukio hilo lililotokea hivi karibuni katika ofisi za Wema zilizopo Mwananyamala jijini Dar kupitia kipindi cha mlimbwende huyo cha In My Shoes, Rado alifafanua:
“Nilimlipa Wema afanye filamu yangu na kabla haijaisha yeye akaenda kutoa nywele na kila kitu bila kuniambia jambo ambalo halitakiwi kwenye filamu ndiyo maana nilifanya vile na siku ile ningemtoa meno,” alisema Rado.