Blogger Widgets

October 15, 2013

Rihanna asababisha kukamatwa kwa mmiliki wa club ya show za ngono, ni baada ya kuitembelea na kutweet maonesho ya watu kufanya ngono live huko Thailand


Tabia ya Rihanna kutembelea club zenye wanawake wanaocheza watupu akiwa Marekani na kueleza kile alichokiona mle ndani kupitia akaunti yake ya twitter, imemponza mmiliki wa bar yenye maonesho ya watu kufanya ngono live huko Thailand baada ya Rihanna kutembelea eneo hilo na kutweet kile alichokuwa anakiona, alivyojisikia na eneo alilopo.Kumbe ilikuwa ni siri na maonesho hayo hayaruhusiwi kisheria nchini Thailand.!
Tweet ya Rihanna iliwashtua Polisi wa Bankonk, na kwa kuwa walikuwa na kila aina ya taarifa kupitia tweet hiyo walimkamata mmiliki wa maonesho hayo na sasa anakabiriwa na kesi ya kujibu mahakamani.

Kiongozi wa ngazi ya juu ya wilaya katika eneo la Bankok Veera Kerdisrimongkol aliiambia AFP kuwa hayo yote yamejulikana baada ya Rihanna kuitembelea sehemu hiyo, na kwamba kuanzia sasa watawabana zaidi watu wenye tabia za kufanya maonesho kama hayo.
comments powered by Disqus