Blogger Widgets

October 15, 2013

Rihanna avunja rekodi Afrika Kusini kwa kuwa msanii mdogo wa kike kujaza uwanja wa mpira, pia amnunulia mama yake nyumba ya bilioni 35.CHECK PICHA

Ile idadi ya watu ambao hufurika katika mechi kubwa za mpira hasa za kimataifa ndiyo ambayo Rihanna aliweza kuikusanya huko Afrika Kusini Jumapili iliyopita.
Rihanna
Weekend iliyopita star wa Barbados aliileta ‘Diamonds World Tour’ Africa, na mashabiki jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini ndiyo waliobahatika kuwa wa kwanza kushuhudia show kali ya hits zake mbalimbali nchini humo.
Mwimbaji wa ‘Diamonds’ Riri amevunja rekodi katika show hiyo ya uwanjani baada ya tiketi zote kuisha kitu ambacho mtandao wa Entertainment Wise unadai hakijawahi kutokea kwa show ya uwanja wa mpira.
Riri-SA
Kwa mujibu wa mtandao wa huo tiketi zote za show hiyo zilimalizika na zaidi ya watu elfu 67 walihudhuria katika show hiyo ya uwanjani na kumfanya Rihanna kuvunja rekodi kwa kuwa msanii mdogo zaidi wa kike wa kwanza kujaza uwanja wa mpira na tiketi zote kuisha.
Hilo lilikuwa ni jambo la mafanikio hata kwa RiRi mwenyewe ambaye alishare habari hizo kwa kutweet
“Rihanna’s show tonight in South Africa will be one of the biggest audiences ever for a female artist and the youngest ever to sellout the stadium.”
Na baadaye alitweet, “Sold out stadium show in #Johannesburg !!! Over 67’000 people #Jah. #histoRIH,”
Rihanna bado yuko Afrika Kusini anakotegemea kutumbuiza jijini Cape Town kesho (October 16)
Tazama baadhi ya picha za Rihanna akiwa ametembelea Zoo nchini humo
Ri-Sa2
Ri-Sa1
Ri-Sa3
Ri-Sa5

Wakati huo huo Rihanna (25) amethibitisha kuwa miongoni mwa wasanii wenye mkwanja baada ya kumnunulia mama yake nyumba ya kifahari kwa dola za Marekani milioni 22 sawa na bilioni 35 za Tanzania huko nyumbani kwao Barbados alikozaliwa na kukulia.
Rihanna-house-1
Riri ambaye hurudi nyumbani kwako kila mwisho wa mwaka kusheherekea sikukuu ya Christmas na familia ameinunua nyumba hiyo ambayo mwaka jana alianza kwa kuikodi kabla hajainunua.
Tazama picha za nyumba hiyo
Rihanna-house-2
Rihanna-house-3
Rihanna-house-4
Rihanna-house-6
Rihanna-house-7
Rihanna-house-8  
From:Bongo5