Blogger Widgets

October 31, 2013

Tatizo Linamkabili Baby Madaha Mpaka Sasa Juu ya Huyu Manager Wake Ambaye Amakuwa Mpenzi wake hivi karibuni

Mwanamuziki na mwigizaji Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, amemshukia mwanamuziki memba mwenzake wa Candy n’ Candy, Top C na kumtaka asimuingilie katika maisha yake. 
 
Kupitia kipindi cha redio hivi karibuni, Top C alisema tangu Baby Madaha asajiliwe katika kampuni hiyo ya muziki iliyopo nchini Kenya, memba wengine wamekuwa wakipuuzwa na bosi wao, Joe Kairuki kiasi kwamba hawasikiki kabisa na kuainisha kuwa Baby anatamba kwa sababu amekuwa ‘kiburudisho’ cha bosi huyo.
 
Alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, Baby alikanusha:
“Top C na wenzake ni wazushi, sina uhusiano na Joe. Mimi nina kipaji kikubwa na nina nidhamu ya kazi kuliko wao ndiyo maana ninapewa nafasi. Wanaendekeza uzushi kwa nini wasipigwe chini?”