Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi
Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.
Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema
(kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza -
Mori jijini Dar.
Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado
yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa
kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki
asubuhi ya leo.Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya
Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na
Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala
kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa
Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani,
lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na
mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti
asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti
yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.
From:Gpl